Header Ads

'Kila mmoja akiwajibika hakuna kisichowezekana kuuhifadhi Msitu wa NGEZI'


Image result for uhifadhi wa Msitu  wa Asili  wa Ngezi (NGENARECO),UWAJIBIKAJI  katika utoaji na upokeaji wa huduma ndio njia pekee Inayotoa  muelekeo kwa Serikali kuweza kuwapatia wananchi maendeleo Yanayostahiki  kwa wakati.

Mwenyekiti wa  jumuiya ya uhifadhi wa Msitu  wa Asili  wa Ngezi (NGENARECO), HASSAN SULEIMAN KHAMIS amesema  kuwa huduma zinaweza kuwa Rahisi na kutolewa kwa wakati jambo ambalo linawezekana  iwapo kila Mmoja atawajibika vyema katika kutekeleza wajibu na majukumu ya kazi Zake.

Kwa upande wake, afisa kutoka Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), BARAKA ALI MBWANA, amesema kuwa, Serikali haina malengo ya kumsumbua Mwananchi kupata huduma bali, bali wanajamii wenyewe wamekuwa Wakichangi kukosa huduma hizo.

Akichangia katika kongamano hilo, UMULHEIR ABAS OMAR, kutoka Tumbe Sekondari, amesema kuwa, kumekuwa na tatizo kubwa la utumikiswaji wa Watoto katika shehia ya tumbe jambo kukithiri kwa utoro wa wanafunzi Maskulini.

Kongamano hilo  limeandaliwa na jumuiya ya uhifadhi wa msitu wa ngezi (NGENARECO) na kuwashirikisha wanajamii wa shehia tofauti pamoja na Watendaji wa mbali mbali wa wa taasisi za  serikali.

No comments