Header Ads

Turin sio mahala salama kwa Real Madrid, Juve wanaweza endeleza rekodi yao nzuri


Baada ya kupita miezi kumi ya siku ile Dunia hasa anga la mjini Cardif kutanda kwa shangwe huku majonzi na machozi ya huruma mithiri ya Nyani aliechoka kukimbia mitini kushuhidiwa ndani ya kikosi cha Massimiliano Alegri, macho na masikio ya mashabeki yanazibuliwa tena usiku huu kushudia vita nyingine kupigwa….
Cristiano Ronaldo hii leo anarejea uwanjani baada ya kupewa mapumziko katika mchezo wa Real Madrid vs Las Palmas, huku Juventus watawakosa Miralem Pjanic na Medhi Benatia ambao wanatumikia adhabu, katika robo fainali ya kwanza kati ya Juventus vs Real Madrid hii leo.
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema hawawezi fikiria yaliyotokea miezi 10 iliyopita katika fainali f huku akitaka vijana wake wacheze kama walivyocheza kipindi cha kwanza katika fainali ya pale Cardiff.
Hii ni kwa mara ya 20 miamba ya soka nchini Hispania Real Madrid watavaana na miamba ya soka ya nchini Italia Juventus, katika mechi hizo Madrid wameshinda michezo 9 huku Juventus wakishinda 8, huku 3 wakienda sare.
Idadi ya mechi ambazo Juve na Madrid wamekutana ni ya pili kwa ukubwa kwani ni Bayern Munich vs Real Madrid(24) pekee ambao wamekutana mara nyingi zaidi kuliko Juve na Madrid katika michuano ya Ulaya.
April mwaka 2013 wakati Bayern Munich wakiifunga Juventus katika michuano ya Ulaya katika uwanja wao wa nyumbani ilikuwa mara ya mwisho kwa Juventus kufungwa kwao katika michuano ya Ulaya, hadi sasa wana mechi 27 nyumbani za Ulaya nyumbani bila kupoteza.
Kwa mara ya kwanza Madrid walimfunga Juve nyumbani mwaka 1962, lakini rekodi ya Juve dhidi ya timu za Hispania katika uwanja wao wa nyumbani ni nzuri ambapo wemeshinda mechi 6 na kusuluhu mechi 1 kati ya mechi zao 7 za nyumbani dhidi ya timu za Hispania.
Japo kuwa 1962 ndio ilikuwa mara ya mwisho kwa Madrid kuifunga Juve mjini Turin lakini vijana wa Zinedine Zidane endapo watafanikiwa kuitoa Juventus katika michuano hii baasi watakuwa wamefanikiwa kutinga nusu fainali ya CL kwa mara ya 13 huku Cr7 akifanikiwa kufunga katika mechi zote dhidi ya Juventus.
SOURCE: SHAFIIDAUDA

No comments