Mkuu wa IMF azitaka Marekani na China kutatua mvutano wa kibiashara kwa kupitia tassisi za pande mbili
MKURUGENZI mtendaji wa
Shirika la Fedha la Kimataifa Christine Lagarde amezitaka Marekani na China
kusuluhisha mvutano wao wa kibiashara kupitia msingi wa kanuni za taasisi za
pande nyingi.
Akizungumza na waandishi wa
habari baada ya mkutano wa kamati ya kutunga sera ya IMF, Bi. Lagarde amesema
Marekani na China zinapaswa kufanya kazi kwa msingi wa biashara huria na ndani
ya mfumo wa msingi wa taasisi za pande nyingi.
Ushauri wa Bi. Lagarde
umekuja wakati waziri wa Fedha wa Marekani Steven Mnuchin akisema kuwa
anafikiria kufanya ziara nchini China ili kujadili masuala ya kibiashara na
wenzake wa China.
Post a Comment