Ajali za barabarani zaua watu 15 nchini Kenya
WATU wasiopungua 15 wameuawa
na wengine zaidi ya kumi wakijeruhiwa katika ajali mbili zilizotokea nchini
Kenya mapema jumapili hii.
Abiria wanane wameuawa na
wengine sita wakijeruhiwa katika ajali kati ya matatu iliyogongana na lori
kwenye barabara kuu ya Mombasa-Nairobi eneo la Mwambi mashariki mwa Kenya.
Kwa mujibu wa kamanda wa
polisi wa kaunti ya Machakos Joseph Tenai, dereva wa matatu alishindwa
kudhibiti gari na kuliparamia lori, jambo lililopelekea watu sita kufariki papo
hapo na wengine wawili walikufa hospitali wakati wakipata matibabu.
Katika ajali nyingine, watu
saba wamefariki baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Probox
kusombwa na mafuriko kwenye kata ya Githabai iliyoko katika jimbo la Kinangop
kaskazini magharibi mwa Kenya kufuatia mvua kubwa zilizonyesha katika maeneo ya
nchi hiyo.
Mkuu wa Polisi nchini Kenya
IGP Joseph Boinnet amewasihi watumiaji wa vyombo vya moto kuchukua tahadhari
katika kipindi hiki ambacho barabara nyingi hazipitiki kutokana na hali mbaya
ya hewa.
CHANZO: CHINASWAHILI
Post a Comment