Wanafunzi Kidato cha Sita Pemba wahimizwa kufuata kanuni za NECTA
KAMATI ya Mitihani Mkoa wa Kaskazini
Pemba imefanya ziara na kuzungumza na wanafunzi wanaojiandaa na mitihani
ya kidato cha sita na kuwasisitiza kufuata kanuni na sheria za baraza la
mitihani .
Katika nasaha zake kwa wanafunzi hao ,
afisa elimu na Mafunzo ya amali Mkoa huo mohammed anassor Salum amesema
mitihani hiyo inaongozwa na kanuni ambazo zinapaswa kuheshimiwa na kuzingatiwa
wakataai wote wa mitihani .
Mohammed amesema baadhi ya
masuala ambayo yamekuwa yakijitokeza kabla na baada ya mitihani ni
vitendo vya udanganyifu unafonywa na wanafunzi.
Naye kamanda wa polisi mkoa huo haji
khamis haji amewataka wanafunzi kujiepusha na vitendo vya udanganyifu ambavyp
vinaweza kuwaharibia malengo yao.
Mwenyekiti wa kamati hiyo bakar ali
bakar amesema mwanafunzi akikamatwa na vitendo vya udanganyifu atakuwa
anaharibu sifa ya skuli yao .
Post a Comment