'Mahujaji Tafteni Elimu ya Hija kuhimili Hija zenu Saudia'

Mahujaji watarajiwa wametakiwa kutafuta
Elimu ya hijaa ili kuweza kujuwa nguzo zake na utaratibu wa ibada hiyo kwa
lengo la kujiweka sawa kiroho na kimwiliili kuweza kuhimili mazingira ya
utekelezaji wa ibada ya hija huko nchini saudi Arabia.
Akitoa semina ya hijja kwa mahujaji
watarajiwa huko Baitul amin Malindi Mjini Unguja Ostadh Khalid Mohd Mrisho amesema
kua ni lazima mahujaji kujiandaa kiroho na kimwili ili waweze kutekeleza
ibadahiyo kwa ufanisi.
Amesema kuwa utakapo pata elimu juu ya
ibada ya hijaa utaifanya kwa mazingatio makubwa zaidi na kujitahidi kutafuta
kiipato kilicho kuwa halali kwa ibada hiyo.
Aidha mahujaji hao wameelezewa kuwa
kufanya ibada hiyo ni kuitikia wito wa Mwenyenzi Mungu kwani ibada hiyo iliaza
wakati wa nabii Ibrahimu [as] pale alipo ambiwa walinganie watu watakuja kutoka
mjini tofauti.
Hata hivyo ostadh amewataka mahujaji
hao kujitarisha katika mambo manene ambayo yataweza kupelekea kukamilika kwa
ibada hiyo kama ilivyo sisitizwa katika Quran.
Nae katibu wa jumuiya hiyo Ali Adam Ali
akiwa nje ya semina hiyo anafafanua malengo ya semina hiyokwa mahujaji.
Semina hiyo ya mahujaji inatarajiwa
kufanyika kwa muda wa siku nne mada tofauti zinatarajiwa kutolewa kawa mahujaji
hawo lengo kuitambuwa kabla y akufika hulo.
Post a Comment