Mtoto Mmoja apoteza Maisha kwa kudaiwa kula Chakula chenye Sumu PEMBA
WATOTO
watatu wakazi wa kijiji cha Kele shehia ya Mtambwe wamefikishwa katika
hospitali ya wete kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kula kitu
kinachosadikiwa kuwa na sumu .
Daktari wa
zamu katika wodi ya watoto katika hospitali hiyo dk Badru Ali Badru
amethibitisha kuwapokea watoto hao na kusema mmoja kati yao alipoteza maisha
wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi , dr Badru amewataja watoto hao kuwa ni AKram
Mohammed Ali mwenye umri miaka 6 na Mula Omar Ali mwenye umri wa miaka 4.
Aidha
dr Badru amesema mtoto Ashraf Husein Hamad mwenye miaka
4 yeye amefariki duni wakati akiendelea kupatiwa matibabu na kusema
wameanza kufanya vipimo vya awali ili kutambua chanzo cha tukio hilo.
‘ Tumeanza
kufanya uchunguzi wa awali kwa kuchukua vinyesi na damu za wagonjwa ili
kuchunguza na kutambua tatizo linalowasumbua watoto hawa‘’alisema .
Akitoa
maelezo kwa katibu tawala , Dk Hawala Saleh amesema tofauti na wakati
wanafikishwa , na baada ya kupatiwa matibabu hali zao zinaendelea vyema.
‘Tofauti
na wakati wanafikishwa hali zao zilikuwa mbaya sana , lakini kwa sasa
baada ya kuwapaatia matibabu hali zao zinaendelea vizuri ’alifahamisha.
Katibu
Tawala wa Wilaya Wete Mkufu Faki Ali amewapongeza madaktari wa hospitali
ya Wete kwa juhudi walizochukua kuokoa maisha ya watoto hao .
Akizungumza
na madaktari na wazazi katika hospitali hiyo , Mkufu amewataka wazazi
kuwafikisha wenye vituo vya afya na hospitali watoto wao wanapohisi wamekula
vitu a ambavyo vinaweza kuleta athari katika maisha yao .
Katibu
Tawala pia katumia fursa hiyo kuiomba Wizara ya Afya kueka chumba maalum
kwa ajili ya wagonjwa waliokatika hali mahututi katika hospitali hiyo ili
kusiwepo na vitendo vya kuwachanganya wagonjwa .
‘Pamoja na
juhudi ambazo madaktari wamezichukua kuhakikisha wanaokoa maisha ya watoto ,
lakini ni vyema Wizara ya Afya kuweka chumba cha wagonjwa mahututi katika
Hospitali hii hususani kwenye kitengo cha watoto ’alishauri.
Hili ni
tukio la kwanza kutokea katika Hospitali hiyo kwa mwaka 2018 kwa watoto
wafikishwa wakiwa wanadhaniwa kula chakula chenye sumu.
Post a Comment