'Wananchi WETE Pelekeni Watoto wenu kupatiwa Chanjo'
WANANCHI wilaya ya wete wametakiwa kuwapeleka watoto wao katika vituo vya Afya kupatiwa
chanjo na kuacha dhana potofu juu ya chanjo hizo .
Kauli hiyo
imetolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Wete Bi Mkufu Faki Ali wakati
akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo katika uzinduzi wa wiki ya chanjo pamoja
na chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi uliyofanyika Junguni wilaya
ya wete mkoa wa kaskzini pemba.
Amesema
Madhumuni makubwa ya wiki ya Chanjo ni kuwakinga watoto
na maradhi mbalimbali yanayowathiri chini ya umri wa
miaka 14 ikiwemo surua,homa ya ini polio pamoja na Saratani ya
Shingo ya kizazi .
Aidha
amesema ni vyema wananchi wa wilaya hiyo kutumia fursa hiyo ili
kuhakikisha watoto wote wanapatiwa chanjo hizo na wale watoto wa kike wenye
umri wa miaka kumi na nne wanafika katika vituo vya Afya mapema kwa ajili ya
kupatiwa chanjo ya kuwakinga na maambukizi ya ugonjwa unaosababishwa na
saratani ya mlango wa kizazi.
Amesema
Serekali ya wilaya itaandaa mikakati na kuhakikisha wanaihamasisha jamii
kushiriki kikamilifu katika zoizi hilo ili lengo la serekali liweze kufikiwa .
Kwa
upande wao madaktari wamesema kuwa chanjo ya Saratani ya shingo
ya kizazi imekuwa ni tatizo kubwa linalosababisha vifo kwa akina
mama.
Post a Comment