Privinvest, ATM zakaribishwa kuwekeza Zanzibar
RAIS wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amezikaribisha
kampuni ya Privinvest na Advanced Marine Transport (AMT), kutoka nchini Dubai
zinazotengeneza meli za aina mbali mbali kuja kuekeza visiwani hapa.
Dk. Shein
aliyazikaribisha kampuni hizo wakati alipofanya mazungumzo wake Jean Boustany
ikulu mjini Zanzibar, aliyefuatana na Balozi mdogo wa Tanzania nchini Dubai,
Ali Jabir Mwadini ambapo mwakilishi huyo alieleza dhamira ya kampuni hizo
kuekeza Zanzibar.
Dk. Shein
alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kutoa ushirikiano na
kuweka mazingira mazuri katika kuhakikisha azma ya kampuni hizo inatimia
kuwekeza hapa Zanzibar.
Alisema azma ya
kampuni hizo imekuja wakati muafaka ambapo Zanzibar imo katika mikakati ya
kutekeleza uchumi wa bahari ambapo hatua hiyo imeonesha mwanzo mzuri kwa
Zanzibar kufikia hatua hiyo.
Aidha,
alimuueleza Mwakilishi huyo kuwa lengo la kampuni hizo kuja kuekeza Zanzibar
itasaidia kuendeleza historia ya Zanzibar ya kuwa kituo kikuu cha biashara
katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati ambapo shughuli hizo zilianza
tokea miaka ya 1899 hapa Zanzibar.
Dk. Shein
alimueleza kiongozi huyo kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari
kushirikiana na kampuni hizo na kueleza hatua itakayofuata kwa viongozi wa
serikali kukaa na uongozi wa kampuni hizo kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa
azma hiyo.
Dk. Shein
alimueleza Mwakilishi huyo kuwa kikao hicho kitasaidia kutoa mwelekeo kwa pande
mbili hizo kutokana na fursa zilizopo sambamba na kuangalia ni uwekezaji wa
aina gani utaanzishwa na kampuni hizo.
Post a Comment