'Wanawake Mjiamini katika Biashara zenu'
WANAWAKE visiwani Zanzibar
wameshauriwa kutumia vizuri fursa ya ujasiriamali kwa lengo la kujiongezea
kipato na kujiajiri wenyewe.
Ushauri huo umetolewa na
Mkurugenzi wa Taasisi ya New Vision Consortium (NVCT) Pily Khamis Lapda,
amesema wanawake wengi hapa nchini wamekuwa wakifanya shughuli za ujasiriamali
kwa mazoea jambo linalopelekea kushindwa kufikia malengo yao ya kumiliki mitaji
mikubwa ya kibiashara.
Amesema zipo njia mbali mbali
za kuwakomboa wanawake kiuchumi zikiwemo kupenda na kuamini shughuli za
ujasiriamali kama nyenzo ya kujikomboa kiuchumi.
Amewashauri wanawake nchini
kujiamini pindi wanapoanzisha biashara zao sambamba na kujiwekea malengo ya
kudumu ya kibiashara yatakayowasaidia kumiliki mitaji mikubwa ya kibiashara.
Mkurugenzi huyo Pily,
akizungumzia malengo ya taasisi yake inayoendesha na kusimamia mafunzo ya
kuyajengea uwezo wa kitaaluma makundi mbali mbali ya kijamii ili
kupata uwezo wa kutumia ipasavyo fursa za ujasiriamali wenye maendeleo.
“Wanawake tuwe mstari wa mbele
kujifunza mbinu mbali mbali za kujikwamua kiuchumi, pia tujitume na kuwa
wabunifu katika biashara zetu ili nasi tuwe miongoni mwa wajasiriamali wa
kimataifa.”, amesema Mkurugenzi huyo.
Akitoa mada ya Uvumbuzi
binafsi, mtaalamu wa Saikolojia na maendeleo ya vijana, Joseph Mrindo amesema
wanawake waliopo katika sekta ya ujasiriamali wanatakiwa kuondokana na dhana ya
ujasiriamali mdogo mdogo kwani hali hiyo inasababisha kudumaa kiakili na
kushindwa kufikia malengo yao ya kumiliki biashara kunwa na makapuni.
Ameeleza kuwa Zanzibar ni
sehemu muhimu yenye fursa za kibiashara hivyo wanawake wanatakiwa kutumia
nafasi hiyo kujiongeza kibiashara.
Mtaalamu huyo, amewasihi
wajasiriamali kufuata maelekezo na mbinu mbali mbali za maendeleo ya kibiashara
ili wawe na mitaji mikubwa itakayowawezesha kupewa mikopo kwa wakati na benki
mbali mbali nchini.
Naye mshiriki wa mafunzo
hayo, Munawar Sleiman Mbarouk amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili wajasiria
mali ni ukosefu wa mitaji na ujuzi wa kufanya biashara
zenye tija kwa mjasiria mali mmoja mmoja na vikundi.
Mafunzo hayo ya siku
mbili yanatolewa na taasisi ya New vision consortium (NVCT)iliyopo Zanzibar na
jumla ya washiriki 200 kutoka taasisi binafsi na za umma wanapewa ujuzi huo wa
ujasiriamali.
Wadhamini wa mafunzo hayo ni
pamoja na NMB, ZSSF, ZURA na IQUITY BANK.
Post a Comment