Simu zatajwa kuwa ndiye 'Mchawi' Bingwa anaeendelea kuvunja ndoa za watu Zanzibar
HUKU jamii ikiwa
na malalamiko ya kuvunjika kwa ndoa hapa Zanzibar, imeelezwa kuwa chanzo
kikubwa kinachosababisha kuporomoka kwa ndoa hizo kwa zaidi ya asilimia 90
kunachangiwa na simu za mikononi.
Kaimu Katibu wa
Mufti wa Zanzibar, ambaye ni mkuu wa Fatwa na Utafiti, Sheikh Thabit Nomal
Jongo, alieleza hayo kwenye mahojiano maalum alipokuwa akizungumza na gazeti
huko ofisini kwake Mazizini.
Sheikh Jongo
alisema ndoa nyingi zinazovunjika Zanzibar kwa zaidi ya asilimia 90, zinatokana
na kuzuka kwa migogoro baina ya wanandoa inayotokana na simu za mikononi.
Alisema, ofisi
yake imekuwa ikipokea kwa jumla wastani wa kesi zisipongua 40 hadi 50 kwa mwezi
za migogoro ya kindoa zinazotokana na simu za mkononi, huku kesi 20 hadi 30 kwa
siku kesi tatu mpaka tano zinahusiana na simu za mkononi.
Aidha, alisema
sababu zinazochangia kuvunjika kwa ndoa hizo kunatokana na wanandoa kutokuwa
wakweli kwenye mawasiliano ya simu zao, hali inayosababisha kujitokeza shaka ya
kuendeana kinyume baina yao na hivyo hatimaye kuamza mgogoro wa kindoa.
Sheikh Jongo
alinukuu maandiko maalum ya kitabu kitukufu cha kur-ani, akisema, “Enyi
mliomuamini Mwenyezimungu mcheni mungu na semeni maneno ya uwazi na ukweli”.
Alifahamisha
kuwa, kwa bahati mbaya wanandoa kabla ya kuoana huwa na mawasiliano
katika mitandao na kuiendeleza wakati wakiwa katika ndoa jambo ambalo linaleta
mfarakano kwa kutoaminiana baina yao.
“Utamuona mtu
ndio kwanza wanaanza maisha katika ndoa anakunywa chai hafla kapigiwa simu
hapokei pale pale ananyuka na kwenda kusikilizia uwani au utamuona anakwenda
kukoga lakini simu yake haiwachi anakwenda kukoga nayo chooni na wengine
huzitia loki simu zao, yote inaonesha dhahiri kuwa watu wamekosa uaminifu”,
alisema.
kusema ukweli
huku akiwasisitiza watu kabla ya kuingia kwenye ndoa kufuta namba ambazo
zinaweza kumletea migogoro na kuweza kuwa huru katika ndoa zao.
Post a Comment