Wanausalama na wanajeshi wapiga kura zao kwa mara ya kwanza kwenye uchaguzi Tunisia
Takriban wanausalama na
wanajeshi elfu 60 wa Tunisia jana walikwenda katika vituo 359 kupiga kura kwa
mara ya kwanza kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Upigaji kura huo umetangulia
kwa wiki moja kabla ya ule wa raia. Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi Bw
Mohamed Tlili Mansri amesema huo pia ni uchaguzi wa kwanza wa serikali za mitaa
kufanyika nchini humo tangu mwaka 2011.
Kura za wanausalama na
wanajeshi zitahifadhiwa kwenye vituo vya kupigia kura, kabla ya kuchanganywa na
kura za raia zitakazopigwa Mei 6.
Kampeni ya uchaguzi wa
serikali za mitaa Tunisia imezinduliwa tarehe 15 mwezi huu na itamalizika
tarehe 4 mwezi ujao.
Post a Comment