Kauli ya Manara kwa YANGA SC, 'Tumewahurumia kwa kuwa nyie ni Mabingwa Watetezi'
AFISA Habari wa
vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC, Haji Manara amefunguka na kudai
kipigo walichokipata Yanga jana Aprili 29, 2018 cha bao 1-0 ni cha heshima
kutokana na wao kuwa mabingwa watetezi hivyo isingekuwa vizuri kuwadharaulisha
mbele ya umati wa mashabiki.
Manara ametoa kauli hiyo mara baada ya ‘Kariakoo Derby’
kumalizika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam huku timu yake ikiwa
imetoka na ushindi wa bao 1 lililofungwa ndani ya dakika 38 kupitia Erasto
Nyoni kwa kutumia kichwa akiunganisha krosi ya Kichuya.
“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumepata matokeo
ila hatujaridhika bado mpaka tuwe mabingwa, ‘perfomance’ yetu kwa ujumla
ilikuwa nzuri ndio maana hata ‘corner’ moja wenzetu hawakuweza kupata lakini
sisi vilevile tulicheza kwa heshima”, amesema Manara.
Pamoja na hayo,
Manara ameendelea kwa kusema “kipindi cha kwanza kilipomalizika nilishuka chini
nikazungumza na wachezaji wangu kuwa waende wakawafunge Yanga kwa heshima
kwasababu wao ni mabingwa watetezi na msiende kuwafunga kwa dharau kwa hiyo
niliwapa maelekezo madhuri vinginevyo tungewadharaulisha kwa kuwafunga mabao 5,
6 kwa hiyo tumewafunga kwa heshima kutokana ni wakubwa wenzetu”.
Kutoka na ushindi
walioupata jana Simba sasa wamekuwa wamefikisha alama 62 kwenye mechi 26 huku
ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja kwenye ligi kuu msimu huu. Simba inabakiza
alama 4 pekee ili iweze kuwa bingwa msimu huu.
Post a Comment