Mahakama yafuta Kesi ya Ubakaji baada ya Mwathirika Kukana Kubakwa KAS PEMBA
BAADA ya
kusota rumande kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili, hatimaye kijana Njile
Masalu Nchilu mkaazi wa Kifumbikai Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba ameachiwa huru na Mahakama ya Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Kijana huyo aliyekuwa
anatuhumiwa kwa kosa la kubaka ameachiwa huru na mahakama hiyo baada ya shahidi
namba moja ambaye ndiye mwathirika wa tukio hilo kukana kufanyiwa kitendo hicho
.
Msichana
huyo mwenye umri wa miaka 15, amekana kufanyiwa kitendo hicho mbele ya hakimu
wa mahakama hiyo Makame Mshamba Simgeni na mwendesha mashtaka wa serikali
Ramadhan Suleiman Ramadhan , jambo ambalo limeifanya mahakama kuliondoa shauri
hilo mahakamani hapo .
Baada ya
mahakama kuliondoa shauri hilo, kijana Njile aliondoka nduki kali katika
viwanja wa mahakama, mithili ya wakimbiaji wa mbio za relay, huku akiwa
haamini kilichotokea.
Njile
alikuwa anakabiliwa na tuhuma ya kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 15,
kosa ambalo alidaiwa kwamba amelitekeleza septemba 5 mwaka 2017.
Post a Comment