RC KAS PEMBA: Ni jukumu la kila Mmoja kudhibiti Mikarafuu Inayopandwa
WIZARA ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
ameshauriwa kuendelea kusimamia agizo la serikali la
kuimarisha zao la karafuu kwa kuhakikisha mikarafuu inapandwa kwa wingi
katika mashamba ya serikali na ya watu binafsi.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini
Pemba, Omar Khamis Othman, wakati akizundua zoezi la upandaji wa
miche ya mikarafuu katika shamba la serikali lililoko Gando wilaya ya
Wete.
Alisema karafuu ni moja ya zao linalosaidia kukuza uchumi wa nchi
na wananchi wake, hivyo ni jukumu la kila mmoja kuienzi na kuitunza mikarafuu
ili iendelee kuchangia pato la taifa.
“Ni jukumu la kila mmoja wetu uhakikisha anasimamia udhibiti wa
mikarafuu inayopandwa ili iweze kustawi na kutumika kwa ajili ya kuchangia
uchumi wa nchi na wananchi wake,” alisema.
Aidha alieleza kwamba kupitia zao la karafuu serikali inapata
fedha za kigeni na hivyo kuchangia maendeleo ya taifa kwa kusaidia miradi ya
maendeleo na huduma za kijamii.
Kaimu Ofisa Mdhamini wizara hiyo, Issa Nasor Ali,
alitaja mikakati inayochukuliwa kukabiliana na upungufu wa mikarafuu ikiwa ni
pamoja na kupanda mikarafuu kwenye mashamba ya serikali.
Post a Comment