Header Ads

'Ugatuzi wa Madaraka Umeboresha Utoaji wa Huduma za Afya kwa Wananchi'- Katibu Mkuu Wizara ya Afya


KATIBU  Mkuu  Wizara ya Afya Zanzibar Bi Asha Ali Abdalla amesema mpango wa ugatuzi wa madaraka kutoka serikali kuu kwenda  serikali za mitaa imesaidia kuboreka kwa utoji wa huduma za afya kwa wananchi .

Amesema tangu Serikali ianze kutekeleza mpango huo huduma za msingi  zimeimarika na hivyo kuwafanya wananchi kuzipata kupitia Halmashauri na Mabaraza ya Miji.

Akizungumza na wakurungezi  wa Halmashauri na Mabaraza ya Miji Pemba  na watendaji  wa  Wizara ya Afya kisiwani hapa katika ukumbi wa maabara ya afya ya jamii  Wawi Chake Chake amewaagiza wakurugenzi kuandaa mipango kazi ambayo itaendana na misingi ya utoaji wa huduma za afya .

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi , Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa , serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Kai Bashir Mbarouk amewataka watendaji wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii ili lengo la Serikali la kutoa huduma bora kwa wananchi liweze kufikiwa .

Mwezeshaji wa kikoa hicho amewataka watendaji wanapopanga mipango yao ya maendeleo kuhakikisha wanazifahamu huduma za msingi amazo zinatolewa kwenye vituo vya msingi ambavyo vimegatuliwa .

Afisa Mdhamini Wizara ya Afya Pemba Bi Shadia Seif  amewataka watendaji hao kushirikiana kwa pamoja ili lengo liliokusudiwa liweze kutekelezwa la kuafikishia huduma wananchi.

No comments