VIJANA PEMBA WAPEWA SIRI YA UZALENDO
Vijana kisiwani Pemba wametakiwa kuwa wazelendo
na Nchi yao Pamoja na kufanya Shughuli za maendeleo kwa faida yao na Taifa kwa
ujumla.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala Wilaya ya
Wete Mkufu Faki Ali alipokuwa akifungua Warsha ya uhamasishaji vijana kujiunga
na vyuo vya amali na elimu mbadala katika ukumbi wa
benjameni Wilaya wete Pemba.
Amesema Vijana ndio nguvu kazi inayotegemewa na
Taifa hivyo ni wajibu wao kutumia muda wao vizuri katika shughuli za kimaendeleo
huku wakijiepusha na vikundi viovu.
Mapema Msaidizi katibu wa jumuia ya uhamasishaji vijana
Mikunguni Asma Ali Makame amesema jamiii imekuwa inakosa uelewa juu ya masuala
ya vyuo vya amali hivyo jumuia yao kwa kuliona hilo ndipo ikandaa warsha ya
uhamsishaji vijana kwa wilaya zote za unguja na Pemba ili kuwahamasisha vijana
kuweza kufahamu umuhimu wa kujiunga na vyuo hivyo.
Nao washiriki wa Warsha hio wamesema mafunzo hayo
yamewasaidia kwani hawakuwa na uelewa wa vyuo vya amali na kuwashauri vijana
walimaliza skuli na hawana kazi waendee kujiunga na vyuo hivyo.
Post a Comment