Karume Boys yapangwa kundi la kifo, yawekwa pamoja na Wenzao Tanzania bara CECAFA
Timu
ya Taifa ya Zanzibar ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 (Karume Boys)
imepangwa katika kundi la kifo kwenye mashindano ya kombe la Chalenji
yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi nchini Burundi April 14 hadi 28, 2018.
Habari
zilizopatikana kutoka kwa CECAFA zinaeleza kuwa Zanzibar
imepangwa kundi ‘B’ pamoja na ndugu zao Tanzania bara, Sudan na Uganda.
Kwa
mujibu wa ratiba iliyotolewa na baraza hilo inaonesha kuwa Zanzibar
itaanza kampeni za kutwaa taji hilo, kwa kucheza na Sudan April 15 katika
uwanja wa Gitega majira ya saa 7:30 za mchana.
Tayari
Zanzibar imechagua wachezaji 20 na ipo katika maandalizi makali chini ya kocha
mkuu Mzee Ali Abdallah, ambapo Vijana hao wapo kambi katika Hoteli ya Zanzibar
Paradise International iliyopo Uwanja wa Amaan.
Katika
Mashindano hayo yamepangwa makundi mawili yani A ambalo lenye timu za Kenya,
Ethiopia, Somalia na wenyeji Burundi.
Michuano
hiyo inatarajiwa kuanza April 14 katika viwanja vitatu tofauti nchini Burundi
vikiwemo uwanja wa Ngozi, Muyinga na Gitega.
Post a Comment