WAFUGAJI KISIWANI PEMBA KUNUFAIKA NA MIPANGO WA IDARA YA MAENDELEO YA MIFUGO
IDARA
ya maendeleo ya mifugo kisiwani Pemba, Imesema inadhamiria kuongeza uzalishaji pamoja
na kipato kwa jamii ya wafugaji kwa kuandaa mafunzo endelevu kwa watoa huduma
za mifugo, kuweza kupandisha mbegu kwa njia ya sindano.
Hayo
yalielezwa na Afisa Mkuu Idara ya maendekleo ya mifugo, ASHA ZAHRAN MUHAMMED,
huko katika kituo cha utafiti wa Mifugo Chamanangwe Wilaya ya
Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Afisa
huyo alisema kuwa, kwa sasa Idara ina mbegu nyingi za kupandishia hivyo
inawataka wafugaji kuwa tayari kupokea huduma kwa kutoa taarifa mapema kwa
maafisa husika kuweza kuwafikia kwa wakati kwa ajili ya kuongeza
uzalishaji kupitia mifugo yao.
Sambamba
na hayo, ASHA alisema kuwa, jamii inatakiwa kuwa a muamko mkubwa kuhusiana na
ufugaji wa Ng’ombe wa kisasa kwani ndio wenye kuingiza faida kubwa iwapo
watapatiwa matunzo yanayostahiki.
‘’Tunataka
wafugaji wabadilike na wasione tabu kutoa taarifa zinazohusiana na mifugo yao
wataalamu wapo, na wako tayari kuwahudumia, wakifanya hivyo basi tunaweza
tukafikia malengo kwa pamoja’’, alisema Afisa Mkuu.
Kwa
upande wake, Afisa Mifugo Wilaya ya Wete , SALUM MUHAMMED SALUM, amewahimiza
wafugaji kutoa ushirikiano kwa maafisa wanapofika kuwapatia huduma huku
akiwataka maafisa hao kujali wakati katika utoaji wa huduma kila
wanapohitajika.
Afisa
huyo alisema kuwa, kila huduma katika suala la mifugo lina nafasi yake hivyo
maafisa wanatakiwa kujali mda wakati wanapopewa taarifa za kuhitajika kwa
huduma, ili kuepusha kuongezeka kwa matatizo pamoja na lawama kwa jamii.
Hata
hivyo, aliwaasa wafuaji kuwa, mbegu zinazopandishwa ni mbeu bora na tayari
zimeshafanyiwa uchunguzi wa kutosha kwa ajili ya kuwasaidia jamii kuweza
kuongeza faida itakayowasaidia kujikimu kwa kuuza maziwa mengi pamoja na
kuongeza mifugo.
‘’Huduma
tunazotoa ni salama kwa ajili ya kuwasaidia wafuji weti waweze kufuga kisasa na
vile wanavovifuga basi ifike siku wapate faida, kwa kuwa shughuli ya ufugaji ni
shughuli ya kujitolea na yenye kazi ngumu’’, alisema SALUM.
Nao
washiriki wa mafunzo hayo, ambao pia ni maafisa wanaeshughulika na utoaji wa
huduma za mifugo, walisema kuwa, wanaimani kubwa ya kufanya vizuri kwa jamii
baada ya kuongeza ujuzi wa kutoa huduma stahiki kwa mifugo.
Maafisa
hao, walisema kuwa nguvu ya pamoja inahitajika kati yao na wafugaji, ili
kufikia lengo lililokusudiwa, huku wakiiomba serikali kupitia Idara ya maendeleo
ya Mifugo, kuwapatia vyombo vya usafiri ambavyo vitasaidia urahisi wa
upatikanaji wa huduma kwa wakati.
Idara
ya mifugo inakawaida ya kutoa huduma ya upandishaji wa mbegu, usafishaji,
pamoja na upimaji wa mimba kwa wanyama, kupitia maafisa wao waliomo katika
vituo vyote vya mifugo kisiwani Pemba.
Post a Comment