Vita ya Mo Salah na De Bruyne yatangazwa, Mchezaji Bora England
Chama cha Wachezaji
wa kulipwa nchini England (PFA) kimetangaza majina ya wachezaji wanaowania tuzo
ya mchezaji bora wa ligi kuu ya EPL msimu huu, ambapo orodha hiyo inaongozwa na
nyota wawili Mohamed Salah na Kevin De Bruyne.
Majina hayo mawili yanapewa nafasi
kubwa ya kushinda tuzo hiyo mbele ya wachezaji wengine wanne waliotangazwa na
PFA kwaajili ya tuzo hiyo ambayo msimu uliopita ilichukuliwa na kiungo wa
Chelsea N'golo Kante.
Manchester City
imeingiza wachezaji watatu katika orodha hiyo ambao mbali na De Bruyne ni Leroy
Sane na David Silva huku mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Harry Kane akiingia
kwenye orodha hiyo kwa msimu wa nne mfululizo.
Mchezaji mwingine
anayekamilisha orodha ya wachezaji sita ni mlinda mlango wa Manchester United
Mhispania David De Gea ambaye amekuwa kwenye kiwango bora katika misimu ya hivi
karibuni.
Wachambuzi mbalimbali
wa soka wanatoa nafasi kubwa kwa Kevin na Salah kutokana na namna
walivyozisaidia timu zao. Kevin ametoa msaada mkubwa kwenye mabao mengi ya Man
City huku Salah akiwa anaongoza orodha ya wafungaji EPL msimu huu akiwa na
mabao 29.
Post a Comment