Wadau wa Soka Micheweni Hamjaona Umuhimu WEMBE STARS....?
TIMU ya Soka ya
WEMBE STARS inayoshiriki Ligi Daraja la Pili wilaya ya Micheweni inakabiliwa na
Changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha kwaajiri ya uendeshaji wa
shughuli za timu hiyo.
Hayo yamebainishwa
katika kikao cha mashabiki, wanachama na viongozi wa timu hiyo kilichokutana
mapema wiki hii kwa ajiri ya kujadili maendeleo ya timu hiyo katika skuli ya
Msingi Maziwang’ombe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Katika kikao hicho
katibu wa timu hiyo, Ali Omar amesema kuwa wameamua kuitana ili kuwekeana
mikakati ambayo itaisaidia timu hiyo kuendelea kufanya vizuri katika ligi
ambayo wanakwenda kushiriki msimu ujao.
Baadhi ya wanachama
walioshiriki kikao hicho wakichangia mada, wameuomba uongozi wa timu hiyo mbali
na ukata wa fedha unaoikabili timu, iunde utaratibu wa kuchangishana michango
kwa mashabiki na wapenzi wa timu hiyo ili kuiwezesha kusonga mbele zaidi.
Katika hatua
nyingine kikao hicho kimeazimia kuwaomba viongozi mbalimbali waliomo katika
wilaya ya Micheweni kujitokeza kujitolea kuichangia timu hiyo ili kuhakikisha
timu inafanikiwa kufuzu kushiriki ligi kuu Zanzibar kwa upande wa Pemba.
Timu ya Wembe Stars
yenye makao yake makuu katika kijiji cha Maziwang’ombe, ilianzishwa mnamo mwaka
1994 na kupewa jina la Wembe Stars kama mwakilishi Pekee katika Wilaya ya
Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Post a Comment