'wauza vyakula zingatieni usafi kuepukana na magonjwa'
WAFANYA biashara za
Vyakula wametakiwa kudumisha Usafi
katika Biashara zao pamoja na
kuvaa Sare ili kuepukana Maradhi ya Mripuko
hususanI kipindupindu.
Akizungumza na wakurugenzi
wa Mabaraza ya miji pamoja na Halmashauri katika ukumbi wa Baraza la Mjii Chake chake Pemba, Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Shamata Shaame Khamis amesema ni vyema Wafanyabiashara za vyakula kudumisha usafi hasa katika kipindi hiki cha mvua za
masika zinazoendelea kunyesha.
Aidha amewata wakurugenzi wa Mabaraza miji
kuhakikisha kuwa wauzaji wa biashara katika maeneo yao wanavaa sare wakati
wakiwa kazini.
Hata hivyo Naibu Waziri
huyo amewaagiza Wakurugenzi hao kusimamia ipasavyo sheria itayokatanza
kudhurura na kuingizwa wanyama katika miji na hata vijijini.
Post a Comment