Header Ads

Zanzibar yafungiwa kwa kupeleka 'vijeba' CECAFA

 
TIMU ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Zanzibar, Karume Boys imefungiwa mwaka mmoja kushiriki michuano ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Cup U17 na kupigwa faini ya dola za Kimarekani 15,000 kwa kosa la kupeleka wachezaji waliozidi umri.

Michuano ya CECAFA Challenge Cup U17 inaendelea nchini Burundi na Zanzibar inadaiwa kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya Januari 1 mwaka 2002, ambao wazi wamezidi umri unaotakiwa wa miaka 17.

Jana timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania Bara, Serengeti Boys ilitoa sare ya 1-1na wenyeji, Burundi katika mechi yake kwanza ya michuano hiyo.


No comments