Header Ads

Afikishwa Mahakamani kwa Wizi wa Bata Wilayani WETE


MKAAZI wa Sebuwatu Shehia ya Bopwe, Bi Amna Khamis Ali 30,  amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Wete akituhumiwa kuiba Mabata Sita.
Imedaiwa mahakamani hapo  na mwendesha mashitaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa mashitaka wa Serikali Juma Ali Juma, mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Abdalla Yahya Shamhuna kwamba mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo tarehe 20/1/2017 .
Amesema kuwa siku ya tukio mtuhumiwa ameiba Mabata sita, majike mawili yenye Rangi Nyekundu na madume manne yote yakiwa na thamani ya shlingi 120,000/- mali ya Seif Hassan Seif .
Baada ya kusomewa shitaka lake, Bi Amina amekana kutenda kosa, huku akiiomba Mahakama impe dhamana ombi ambalo limekubaliwa mahakamani hapo.
Mtuhumiwa yuko nje  baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambapo ametakiwa kujidhamini mwenyewe kwa shilingi 70 za maandishi na mdhamini mmoja.

No comments