'Wananchi Pemba toeni mashirikiano kwa watafiti wa Mafuta, Gesi'
WANANCHI kisiwani
Pemba wametakiwa kutoa mashirikiano na kukubali kuruhusu maeneo yao kutumika wakati wa kazi ya utafiti wa mafuta na gesi
asilia unapofanyika.
Meneja mkuu wa
kampuni ya utafifi wa mafuta na gesi asili ya BRUNSWICK RESOUCES LIMITED Steven
Lwendo ameyasema hayo huko ukumbi wa Taasisi ya nyaraka na Mambo ya kale Chake –chake Pemba alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari juu kutoa elimu kwa jamii kuhusu zoezi la
utafiti ilinavyoendele.
Amesema ni lazima
watu waelewe kinachoendelea katika zoezi hilo ili kujenga matumaini juu ya kazi
hiyo.
Awali Afisa
Mdhamini wizara ya Maji Ujenzi Ardhi na Nishati Juma Bakari Alawi amesema
wananchi wanapaswa kuwa watulivu na kusikiliza maelekezo ili kurasihisha
utafiti huo kufanyika kwa mafaniki.
Nao waandishi hao
wameahidi kushirikiana na mamlaka na watafiti hao ili kuwapa taarifa wananchi
kila eneo ambalo utafiti unafanyika
Post a Comment