WHO yawatahadharisha watalii wa kimataifa kuhusu mlipuko wa Ebola DRC
SHIRIKA la afya duniani WHO
limewatahadharisha watalii wa kimataifa kuhusu mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri
ya kidemokrasia ya Kongo DRC kutokana na mwelekeo mpya wa homa hiyo.
Shirika hilo limesema kwa
ujumla hatari ya maambukizi ya homa ya Ebola kwa watalii nchini DRC ni ndogo,
kwa kuwa wagonjwa wanaweza kuambukiza wengine baada ya kuonesha dalili ikiwa ni
pamoja na homa, kukosa nguvu, maumivu ya misuli, kichwa na koo.
WHO imewashauri watalii
wanaotaka kwenda DRC kutafuta ushauri wa kidaktari zaidi ya wiki nne hadi nane
kabla ya safari.
Ushauri huo, ni pamoja na hatari za
kiafya, mahitaji ya chanjo na dawa za malaria, pamoja na vitu vingine vya
matibabu vinavyohitajika.
Post a Comment