DC Micheweni: 'Tunaendelea kutatua tatizo la Maji Micheweni'
TATIZO la uhaba wa
Maji linalowakabili wananchi wa Shehia za Majenzi Wilaya ya Micheweni limeanza
kutafutiwa ufumbuzi baada ya zoezi la uwekaji wa Mifereji ya Maji na Matanki
katika Maeneo hayo kuanza.
Akizungumza na
Wananchi wa Shehia ya Majenzi Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Salama Mbarouk Khatib
amesema Serikali ya Wilaya imesimamia kero za Wananchi walizozotoa wakati
alipokuwa akifanya mikutano ya Shehia.
Salama amesema
matatizo ambayo yameelezwa katika shehia tayari ameanza kuyafanyia kazi ili
kuhakikisha wananchi wananufaika na Serikali yao chini ya Rais. Dok. Ali
Mohamed Shein.
Nae Mkurugenzi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hii, Hamad Mbwana Shehe amesema Serikali
imejipanga kuhakikisha kwamba tatizo la Maji katika Wilaya ya Micheweni.
Amesema kuwa fedha hizo
ni miongoni mwa makusanyo yanayokusanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni
kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake.
Kwa upande wake
Sheha wa Shehia hiyo, Fakh Kombo Hamad, amesema wamefurahishwa na kitendo cha
Serikali ya Wilaya kuwatatulia kero hiyo ya Maji katika Shehia yake.
Post a Comment