Walimu wakuu Skuli za Msingi Watakiwa kuongeza Uwajibikaji
KAIMU Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete
Bi Salma Abuu Hamad amewataka walimu wa wakuu wa skuli za msingi kuongeza
uwabikaji katika kusimamia maendeleo ya elimu katika skuli zao ili kuongeza
ufaulu wa wanafunzi .
Akizungumza na walimu wakuu wa skuli za
msingi ambazo zimeinga kwenye mpango wa Serikali wa Ugatuzi , Kaimu Mkurugenzi
amesema ni vyema walimu wakuu kuwa makini katika kuwasimamia walimu wao kwani
kuongezeka ufaulu wa wanafunzi ni sifa kwa mwalimu.
Naye Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Fundi
Msingi Maulid Ali Salim amuomba uongozi wa Baraza la Mji Wete kuandaa utaratibu
wa kuwalipa posho walimu wanaojitolea ili wasivunjike moyo na waendelea
kuwasaidia wanafunzi.
Afisa Elimu na Mafunzo ya Amali Mkoa wa
Kaskazini Pemba Mohammed Nassor Salim dhamira ya Serikali wa kuzigatua baadhi
ya taasisi ni kuleta usimamia imara wa utoaji wa huduma bora .
Post a Comment