DC WETE azionya Asasi za Kiraia Wilayani humo zitakazofanya kazi Kisiasa,
MKUU
wa Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali amezitaka asasi za kiraia katika wilaya hiyo
kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kujiepusha na masuala ya kisiasa ndani
yake.
Hayo
ameyasema wakati akifungua kongamano ya haki za binadamu linaloendeshwa na
muungano wa asasi za kiraia pemba -PASCO-
Amesema
anaendelea kuzifuatilia asasi za kiraia na akibaini kwamba asasi ambayo
itajihusisha na siasa ataisimamisha kwa kuwa itakuwa inakwenda kinyume na
sheria za kuanzishwa kwake.
aidha
mkuu huyo wa Wilaya amesema washiriki wa mafunzo hayo wajenge uzalendo na
kuweza kuisaidia nchi yao ili kuendelea kudumisha amani iliyopo hapa nchini.
Nao
washiriki wa kongamano hilo wameushauri uongozi wa asasi hiyo , kufika maeneo
ta vijijini kwa ajii ya kutoa elimu kwa wananchi ili kusiwepo na vitendo vya
ukiukwaji wa haki za bnadamu .
Post a Comment