Pombe haramu ni tishio MICHEWENI, Msako wa DC Wabaini mengine tena
DUMU
11 zinazosadikiwa kuwa ni Pombe haramu aina ya Gongo zimekamatwa katika Shehia
ya Kiuyu Kipangani, Wilaya ya Micheweni zikiwa zimefukiwa ardhini baada ya
kufanyika kwa Oparesheni ya kupambana na dawa za kulevya Wilayani hapa.
Kwa
mjibu wa taarifa kutoka kwa Mkuu wa
Wilaya hiyo Bi Salama Mbarouk Khatib amesema kuwa katika oparesheni hiyo pia wamefanikiwa
kukamata tangi moja la Maloweko yaliyokuwa yanaandaliwa kwa ajili ya
kutengenezea Pombe hiyo.
Mkuu
wa Wilaya ya Micheweni Bi. Salama Mbarouk Khatib akishiriki zoezi la Ufukuaji
wa Madumu ya Maloweko ambayo yamekutwa yamefichwa Ardhini wakati wa Oparesheni
hiyo
|
Aidha
Salama amewataka wananchi kuendelea kutoa mashirikiano kwa Jeshi la Polisi pamoja
na Polisi jamii pindi wanapoona viashiriavya matendo hayo katika jamii zao ili
kuhakikisha Pombe hizo zinatokomezwa.
Kwa
mjibu wa Mkuu wa Wilaya hiyo watuhumiwa wawili wamekamatwa katika Oparesheni
ambao ni Hamad Rashid Ali (23), Mkaazi wa Kipange pamoja mwenzake aliyefahamika
kwa jina moja la Paulo na tayari wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi
zaidi.
Madumu yaliyokamatwa katika oparesheni yakishishwa kituo cha Polisi Matangatuani. (PICHA ZOTE NA GASPARY CHARLES)
|
Oparesheni
hiyo ya kupambana na Dawa za kulevya Wilaya ya Micheweni ni mwendelezo wa
oparesheni inayoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambae pia
ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Salama Mbarouk Khatib kwa kushirikiana na Polisi
Jamii.
Post a Comment