Ligi Kuu Pemba yafikia tamati
LIGI Kuu ya
Zanzibar kanda ya Pemba ilifikia tamati juzi ambapo Opec ilifanikiwa kuilaza
Wawi Star magoli 3-1 kwenye uwanja wa Gombani.
Ushindi huo
uliiwezesha Opec kufikisha pointi 49 na kushika nafasi ya pili nyuma ya Mwenge
yenye pointi 50.
Timu hizo
zilianza mchezo kwa ushindani mkubwa huku kila upande ukikosa mabao ya wazi na
kujikuta zikienda mapumziko zikiwa hazijafungana.
Lakini, kipindi
cha pili kilianza kwa mshike mshike na Opec kuonekana kulisakama lango la
wapinzani wao kama nyuki na kufanikiwa kupata goli la kwanza lililofungwa na
Morris Rauri kwenye dakika ya 50.
Mshambuliaji,
Khamis Sadik aliifungia Opec goli la pili kwenye dakika ya 64 kabla ya Wawi
Star kufunga la kufutia kupitia kwa Mohamed Haji katika dakika ya 66.
Kila muda ulipokuwa
ukiyoyoma huku mvua zikiendelea kunyesha,mshambuliaji Moris Raul kwa mara ya
pili alizifumania nyavu za Wawi kwenye dakika ya 86 na kuandika bao la tatu.
Post a Comment