Miti 2,000 kupandwa Wilaya ya Micheweni kurejesha uhalisia wake
JUMLA ya
miti 2,000 za Matunda na Biashara inatajiwa kupandwa kwenye eneo la Mamoja
Wilaya ya Micheweni ambalo limeathirika kutoka na uchimbaji wa mchanga.
Eneo hilo
lenye ukubwa wa hekta 16.5 , litapandwa miti ili kurejesha uhalisia wake ambao
umepotea kutokana na matumizi makubwa ya mchanga yasiyozingatia hifadhi ya
mazingira.
Akizungumza
wakati wa zoezi la upandaji wa miti katika eneo hilo , Kaim Afisa Mkuu wa Idara
ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka Pemba Mussa S aid Bakar amesema asilimia
kubwa ya miti hiyo inaweza kusaidia wanajamii katika shughuli za kiuchumi.
Amesema jamii
inataakiwa kuwa mstari wa mbele kusimamia uhifadhi ya misitu na mazingira kwa
kuitumia rasilimali ya miti kwa utaratibu ili kuepusha uharibifu unaweza
kujitokeza na kuleta athari wa jamii.
''Katika
eneo hili tunatarajia kupanda miti 2000 ya matunda na misitu na ambayo
itawanufaisha wananchi wa eneo hili na hivyo kukuza uchumi wao na familia zao,''
alisema.
Mussa
amesema kuwa ni jukumu la kila mwananchi kushiriki kuyalinda na kuyatunza
mazingira kwa kujiepusha na ukataji wa miti ovyo ili kudhbiti athari za
kimazingira .
Mmoja wa
vijana kutoka baraza la vijana shehia ya Shumba, Mohammed Salim Tall amesifu
hatua zilizochukuliwa na Idara ya Misitu kupanda miti katika eneo hilo na
kuahidi kushiriki katika kuilinda na kuitunza miti hiyo.
Tall amesema
kuharibiwa wa eneo hilo kutokana na matumizi ya binadamu , kumeleta athari kuwa
kwa jamii kwani hata sehemu ya malisho ya mifugo imepotea .
''Sisi
Vijana tuta shirikiana na Idara kuilinda na kuitunza miti iliyopandwa kwani
watakaonufaika ni sisi ni sio watendaji wa Idara, '' alifahamisha.
Naye Tune
Haroub Juma amewasisitiza wananchi kuepusha na vitendo vya kukata miti ovyo
pamoja na kuchimba mchanga kwa ajili ya kulinda vitendo vya uhalifu wa
mazingira.
Tune
ameitaka jamii kuzingatia kauli mbiu ya panda miti kata mti , na kuhakikisha
maeneo yote yanabaki kwenye uhalisia na uoto wake wa asili.
''Tuzingatie
kauli mbiu ya panda miti kata mti ,lengo ni kudhibiti uharibifu wa mazingira na
kurejesha uhalisia wa uoto wa asili '' alifahamisha.
Katika zoezi
hilo na upandaji wa miti , jumla na miti 400 aina ya mikorosho imepandwa
katika eneo lenye ukubwa na hakta 2.5.
Post a Comment