Walimu Elimu Mbadala waomba kuongezewa Mafunzo zaidi
WALIMU
wanaosomesha Elimu Mbadala na watu wazima wameitaka Idara Elimu Mbadala
na watu wazima kuendelea kuwapatia mafunzo ili waweze kutekeleza kazi zao kwa
ufanisi.
Walimu
wa kituo cha Elimu Mbadaka Wingwi wilayani hapa wamepongeza uamuzi wa Idara
hiyo wa kuwapatia mafunzo ambayo yatawajenga uwezo na kuboresha kazi zao .
Mwalim
Ameir Ali amesema mafunzo aliyoyapata yamemsaidia kuweza kufahamu mbinu za
kufundisha pamoja na kupata taaluma ya saikolojia ya kuweza kumsaidia
mwanafunzi mtu mzima.
NAye
Mwalimu Halima Abdalla amesema mafunzo hayo ni dira katika kuongeza uwezo na
ufahamu wa kutoa huduma kwa wanafunzi .
Naye
Mwalimu Haji Omar Ali kutoka Idara ya Elimu Mbadala na watu wazima Pemba
amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha walimu kupata taaluma na mbinu
mbadala za kuweza kuwafundisha wanafunz watu wazima .
Post a Comment