MSUVA: Nitacheza na SAMATTA
WINGA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Simon Happygod Msuva
amekubali kuchezea kikosi cha Marafiki wa Mbwana Ally Samatta katika mechi
maalum ya hisani dhidi ya Timu ya mwanamuziki Ali Kiba na rafiki zake
kuhamasisha uchangiaji wa vifaa na miundombinu mashuleni Juni 9, mwaka huu
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na Vyombo vya habari winga huyo mwenye kasi Msuva amesema kwamba anaunga mkono kampeni hiyo na atakuwepo Juni 9 kucheza mechi hiyo maalum ya Hisani.
Mratibu
wa mechi hiyo, Daniel Cleverest amesema kwamba maandalizi yanaendelea vizuri na
mgeni rasmi siku hiyo anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Dk. Harrison George Mwakyembe.
Post a Comment