Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Marekani wakutana
WAZIRI wa mambo ya nje wa
China Bw. Wang Yi amekutana na mwenzake wa Marekani Bw. Mike Pompeo mjini
Washington na kubadilishana naye maoni kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili
na masuala wanayofuatilia kwa pamoja.
Bw. Wang amesema ni muhimu
kudumisha uhusiano mzuri kati ya China na Marekani, kuimarisha ushirikiano wa
kusaidiana, kutatua tofauti na masuala kwa njia mwafaka na kupanua ushirikiano
katika masuala ya kikanda na kimataifa.
Kwa upande wake Bw. Pompeo
amesema Marekani inapenda kushirikiana zaidi na China, na kwamba rais Donald
Trump anathamini sana uhusiano mzuri wa kikazi na urafiki binafsi kati yake na
rais Xi Jinping wa China. Ameongeza kuwa katika suala la Taiwan, Marekani
inashikilia msimamo wa kuwepo kwa China moja.
Katika suala la uchumi na
biashara, amesema hivi karibuni vikosi kazi vya kiuchumi vya Marekani na China
vilifanya majadiliano ya kiujenzi na ameeleza matumaini yake kuwa nchi hizo
mbili zinaweza kubainisha na kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na
kuwanufaisha wananchi wao.
Post a Comment