Waziri SMZ: Fedha za TASSAF hazihusiani na Siasa
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamo
wa Pili Mhe Mohamed Aboud Mohammed amesema Fedha za Ruzuku zinazotolewa na
mfuko wa maendeleo ya Jamii nchini TASSAF kusaidia kaya maskini hazihusiani na
maswala ya kisiasa.
Akizungumza na masheha wa
wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, Madiwani pamoja na watendaji wa Serikali katika ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, amesema wanufaika wa fedha hizo ni wananchi waliotimiza
vigezo bila ya kujali itikadi ya vyama vyao.
Aidha amesema kuwa Serikali
haina nia ya kumtenga mwananchi kutokana na imani yake kisiasa juu ya Ruzuku hizo
bali itaendelea kusimamia haki kwa wananchi wote.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini
mhe Omar Khamis Othman amewasisitiza masheha kuacha kuwabagua wananchi kwa
misingi ya kisiasa kwani fedha hizo zinatolewa kwa wananchi wote wa Zanzibar
waliotimiza vigezo.
Post a Comment