Wananchi Micheweni watakiwa kushirikiana na Watafiti wa Mafuta Wilayani humo
MASHEHA Wilaya ya
Micheweni wametakiwa kutoa elimu ya utafiti wa uchimbaji wa mafuta na Gesi kwa
Wananchi ili kuweza kuvitunza na kuvilinda vifaa vya utafiti ambavyo vitawekwa
katika Maeneo yao.
Ushauri huo
umetolewa na Afisa Mdhamini Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Pemba,
Juma Bakar Alawi katika kikao cha kuitambulisha Kampuni ya Utafiti wa Mafuta na
Gesi ya BGP kwa Masheha wa Wilaya hiyo.
Mdhamini huyo
amesema ili zoezi la Utafiti wa Mafuta na Gesi liweze kufanikiwa kwa kuwango
sitahiki ni lazima Masheha kuwa Msitari wa Mbele kutoa Mashirikiano kwa Kampuni
hiyo ikiwa ni pamoja na kuwashajihisha wananchi wao kuilinda Miundombinu ya
Utafiti huo.
Awali akizungumza
katika kikao hicho, Afisa Rasilimali Watu wa Kampuni hiyo, Abdul Bashiru
Mohamed amesema zoezi hilo linatarajia kutoa fursa za Ajira kwa Wananchi
mbalimbali.
Post a Comment