DC Micheweni awaonya Watendaji 'Ndumi Kuwili' Ofisini Kwake
WAFANYAKAZI
wa Ofsi ya Mkuu wa Wilaya ya Micheweni wametakiwa kutunza siri za ofsi na
kufanya kazi zao ambazo wamelekezwa kwa mujibu wa sheria za utumishi wa Umma.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Salama Mbarouk Khatib wakati alipokuwa
akizungumza na Watendaji hao ofini kwake.
Amesema
mfanyakazi ambaye anatowa siri za ofsi inakuwa huyo simuadilifu na baadala yake
hata nyaraka za ofsi anaweza kuzitowa nje.
Aidha Salama
amewataka wafanya kazi hao kujituma katika nafasi zao ili kuweza kuiletea
maendeleo wilaya kwani wao ndio kioo cha jamii inayowazunguka.
Naye katibu Tawala Wilaya hiyo Hasani Abdalla Rashid amesma katika utendaji hatamuonea
haya mfanyakazi ambaye atashindwa kufanya majukumu yake.
Amesema
hapendi kuona mfanyakazi anapokuja ofsini anakuwa na vikundi vya mazungumzo na
baadala yake kuacha kazi ambayo amepangiwa.
Baadhi ya
wafanyakazi katika Ofisi hiyo wamepongeza hatua ya viongozi wao kuwahimiza
majukumu yao kwani kunabaadhi hawafahamu majukumu yao Ofisini hapo.
Post a Comment