Pemba: Tatizo la ajira kwa watoto Mwiko, Watoto 360 Warejeshwa Skuli
JUMLA ya watoto 360 waliokatisha masomo na kujiingiza
katika ajira za utotoni Shehia ya kiwani Mkoa wa kusini Pemba wamefanikiwa
kurejeshwa Skuli na vyuoni baada ya wazazi wao kuamua kuanzisha ulinzi
shirikishi(Polisi jamii).
Akizungumza na REDIO JAMII MICHEWENI huko kijijini
kwao mmoja miongoni mwa polisi jamii Mohd Hamrani Awesi amesema sababu
iliyopelekea kuanzishwa kwa ulinzi shirikishi katika shehia yao ni kutokana na
madhila kuwa makubwa,kukithiri kwa ulevi,wizi pamoja na kundi kubwa la watoto
kukatisha masomo na kujiingizaa katika ajira mbaya za utotoni za uvuvi.
Amesema hadi kufikia sasa ambapo ni takribani mieze 8
tokea kuanzishwa kwa ulinzi shirikishi wamefanikiwa kirejesha skuli na vyuoni
watoto 360 ambao tayari walikuwa washakatisha masomo.
Amesfahamisha kuwa licha kufanikiwa kwa kiasi kikubwa
katika kuwatoa watoto katika ajira mbaya za utotoni lakini hadi kufikia sasa
bado kuna baadhi ya watoto hawajafanikiwa kuwarejesha skuli hii ni kutokana na
wazazi wao kutotoa ushirikiano wakutosha.
''Licha ya kazi kubwa tunayoifanya ambayo inamaslahi
kwa jamii na watoto wenyewe juu ya kapata haki yao ya msingi ya Kielimu lakini
wapo baadhi ya wazazi hawapendi kabisa kuona juhudi hizi zinafanyika na wengine
hadi kufikia kutupangia hujuma pamoja na vitisho mbalimbali lakini sisi
hatujali kwani lengo letu ni kuleta ukombozi kwa jamii.'' ameeleza Hamrani.
Baadhi ya akina mama wa shehia hiyo wamesema wanashukuru
na sana kuanzishwa kwa polisi jamii kwani imekuwa ikiwasaidia ulezi kwa kiasi
kikubwa na kusema kuwa hadi sasa watoto ambao tayari walikuwa wameshindikana
wameweza kurejeshwa skuli na vyuoni.
Kwa upande wake sheha wa shehia ya Kiwani Abdallah
Makame Hamad amesema moja ya malengo makuu ya kuanzishwa polisi jamii ni
kuhakikisha kila mtoto mwenye haki ya kupata elimu anaipata na kusema
kuwa katika shehia yake kuna tatizo kubwa la kutokuwepo kwa vijana waliosoma.
Ameeleza kuwa sasa wamepiga hatua kubwa ya kimaendeleo
kwani kundi kubwa la watoto waliotoroka skuli wamefanikiwa kuwarejesha,
kudhibiti masuala ya ulevi, watoto kwenda uchi pamoja na mikato ya ajabu kwa
vijana.
Amefahamisha kuwa licha hatua kubwa ya maendeleo
yaliyoipiga lakini pia kumekuwa na changamoto kubwa ambazo zinaikumba polisi
jamii na kusasababisha kutofikia malengo yake waliyojipangia na kuzitaja kuwa
ni pamoja na uhaba wa vifaa, kama vile tochi, usafiri, viatu pamoja na
kukosekana hata pesa kidogo kwa ajili ya watu wanafanya kazi hii ya ulinzi
shirikishi.
Aidha ameiomba serikali na taasisi binafsi kujitokeza
kuwaunga mkono kwa kuwasaidia kuwapatia vifaa vitakavyo saidia kufikisha
shebaha yao sambamba na hayo amewaomba wazee wale ambao hadi sasa wanakuwa na
fikra kuwa polisi jamii zinawaonea watoto wao kuachana na fikra hizo potofu na
badala yake kuungana kwa pamoja katika kuleta mabadiliko ya kielimu katika
sehia yao.
Post a Comment