China yaipongeza Burkina Faso kukata "uhusiano wa kibalozi" na Taiwan
MSEMAJI wa Wizara ya Mambo ya
Nje ya China Bw. Lu Kang amesema China inapongeza uamuzi wa Burkina Faso kukata
"uhusiano wa kibalozi" na Taiwan.
Bw. Lu amesema inajulikana
duniani kuwa mwezi Oktoba mwaka 1971, kikao cha 26 cha Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa kilipitisha Azimio Nambari 2758 na kuweka bayana kuwa serikali ya
Jamhuri ya Watu wa China ni serikali pekee halali inayoiwakilisha China.
Ameongeza kuwa mkutano wa
kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utakaofanyika
mwezi Septemba mwaka huu utafanya ushirikiano wa kirafiki kati ya pande hizo
mbili ufikie kwenye ngazi mpya.
Amesema China inaikaribisha
Burkina Faso kujiunga na ushirikiano huo mapema iwezekanavyo, kwenye msingi wa
kanuni ya kuwepo kwa China moja.
Post a Comment