'Masheha, Jeshi la Polisi Shirikianeni kutokomeza Uharifu Micheweni'- DC Salama
MASHEHA pamoja na Jeshi la Polisi Wilaya ya Micheweni wametakiwa kufanya kazi kwa mashirikiano
ili kupambana na matendo ya kihalifu ambayo yanafanywa na wananchi katika
shehia zao.
Ushauri huo
umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Micheweni Bi Salama Mbarouk Khatib katika ukumbi
wa mikutano wa skuli ya Micheweni Sekondari wakati alipokuwa akizungumza na
masheha pamoja na polisi wa shehia waliomo ndani ya wilaya hiyo.
Amesema jeshi la Polisi endapo litafanya kazi kwa
karibu na kushirikiana na masheha matendo mbalimbali ya kihalifu yatapungua
katika wilaya ya Micheweni.
Kwa upande wake Mkuu
wa upelelezi wa Makosa ya jinai Wilaya hiyo Mussa Khatib Vuai ambae pia ni
kaimu Mkuu wa Polisi wilaya hiyo amesema usalama wa nchi yeyote unahitaji
mawasiliano ya karibu kati ya taasisi na taasisi, hivyo ni budi kwa masheha
kufanya mawasiliano ya karibu na jeshi la polisi pindi tu matukio yanapotokea.
Amesema masheha ni
jukumu lao kufanya vikao kwa kushirikiana na askari wa shehia zao ili
kuhakikisha wanaandaa mikakati madhubuti ya kupambana na wahalifu katika shehia
zao.
Post a Comment