Header Ads

Wananchi Micheweni Wachekelea Mafunzo ya Mkataba wa Afrika juu ya Utawala Bora, Uchaguzi na Demokrasia


ActionAid International 
WANANCHI wametakiwa kuyapokea vyema na kuyafanyia kazi mafunzo ambayo wameyapata juu ya Mkataba wa Afrika juu ya  Utawala Bora, Uchaguzi na Demokrasia kupitia mradi wa ACTION AID ili kuweza  kunufaika.

Hayo yameelezwa na Rashidi Hassani Mshamata  Kutoka katika jumuiya ya walimu wa Uraia  Tanzania Tawi  la Pemba alipokua akitoa Elimu kwa wananchi juu mkataba huo.

Naye Maryam Ramadhan Khamis mkazi wa kijiji cha Tumbe Mashariki ameeleza kuwa wameyapokea mafunzo hayo kwa furaha kubwa kwani wamefaidika vya kutosha juu ya mambo ambayo walikua hawayajui.

Kwa upande wake Yahya Ali Hamad ameeleza kufurahishwa kwake na mafunzo hayo na ameiomba serikali kujiunga na mkataba huo kwani unafaida nyingi kwa jamii na nchi kiujumla.

Amesema atakua Balozi mzuri wa ActionAid kwa kutoa elimu kwa wananchi wengine juu ya mafunzo hayo na kuiomba jamii kuepukana na maneno ambayo hayafai juu ya mradi huo.

Mafunzo hayo ni muendelezo wa mafunzo ya wananchi kwa Wilaya ya Micheweni juu ya Mradi wa Action Aid ambayo yanaendeshwa na wafanyakazi wa Shirika hilo.

No comments