Wavuvi Kisiwani Pemba walia na Uvuvi haramu
BAADHI ya Wavuvi kisiwani Pemba
wamesema kuwepo na wavuvi wanaoendelea kutumia dhana haramu kunachangia
kupungua kwa mazao ya baharini wakiwemo Samaki.
Akizungumza na REDIO JAMII MICHEWENI,
Mohammed Ali Kombo amesema Uvuvi wa kutumia Nyavu za kukokota unaathari kimazingira
kwani husababisha Samaki wadogo nao kuvuliwa .
Aidha amesema aina nyengine ya Uvuvi ya
kutumia Mabomu huwakimbiza Samaki na hivyo kuwaathiri kiuchumi wavuvi .
Afisa Mkuu wa Idara ya Uvuvi na Mazao
ya Baharini Sharrif Mohammed Faki amewataka wavuvi kujiepusha na Uvuvi haramu
ili waweze kuyalinda Mazingira.
Faki amewataka wavuvi kuithamini kazi
yao hiyo kwani ndiyo inayowaangizia kipato kwa kuhakikisha wanafuata taratibu
na sheria zilizowekwa .
Mpaka sasa tayari Idara hiyo imeanza kuchukua
juhudi mbalimbali ikiwemo kutoa Elimu kwa wavuvi kupitia kamati za wavuvi
kutambua athari za kutumia dhama haramu.
Post a Comment