Serikali ya wilaya ya Micheweni yahimiza upandaji wa miti
Jumla ya miti 3000
msitu imepandwa kando kando ya bara bara katika shehia ya mtemani wingwi ili
kuzuwia mmonyoko wa ardhi.
Akizungumza wakati
wa zoezi hilo afisa mipango wilaya ya micheweni ndugu hamad Othamn Khamis kwa
niaba ya mkuu wa wilaya hiyo ametaja faida za mti hiyo ni pamoja na kuzalisha
hewa kwa ajili ya viumbe hai.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa halmashauri Omar Issa Kombo, asmeitaka jamii kujenga utamaduni wa
kupandamiti katika maeneo yao ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Akizungumza na
redio jamii baada ya zoezi hilo mwanafunzi Omar Juma Mbarouk kutoka wingwi
secondary ameahidi kushirikiana na wana jamii katika kuilinda miti hio.
Kwa mujibu wa
taarifa kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya nikwamba zoezi hilo litakua endelevu
ambapo lengo lake ni kurejesha uoto wa asili.
Post a Comment