Wakala wa Chakula, Dawa na Vipondozi Pemba yabaini Kiwanda 'Feki' Mkoani
WAKALA wa Chakula , Dawa na Vipondozi
Ofisi ya Pemba imewatoa hofu wananchi kwamba katika kipindi hichi cha mwezi wa
Ramadhan wataendelea kutumia vyakula ambavyo viko salama kwa maisha yao .
Akizungumza ofisini kwake Juma
Seif Khamis amesema katika ukaguzi walioufanya wamebaini kuwepo na kiwanda cha
Tambi Wilaya ya Mkoani ambacho kinatumia Unga uliopitwa mataumizi yake .
Amesema hatua ambazo wamezichukua
ni kuzuia matumizi ya Unga huo pamoja na tambi ambazo zilikuwa zimetengenezwa
ambapo kwa sasa zinatarajia kuangamizwa.
Aidha kwa
upande wake Mohamed Said Abdalla afisa kutoka wakala amesema kwamba tayari
imeanza kufanya ukaguzi katika maduka , bandarini pamoja na kudhbiti misaada
ambayo inatolewa na wahisani katika kipindi hichi na kuifanya uchunguzi kabla
haijawafikia wananchi
Post a Comment