Header Ads

MAPATO YA SOKO LA TUMBE WILAYA YA MICHEWENI KUWANUFAISHA WANANCHI WA ENEO HILO


Uongozi wa halmashauri ya wilaya ya micheweni umesema utaratbu kwa ajili ya mgawanyo wa mapato katika soko la samaki na mboga mboga tumbe uliandaliwa kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi wa tumbe .

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo  hamad mbwana shehe amesema halmashauri ilipingana na kauli za baadhi ya wananchi wa tumbe za kuzihifadhi fedha majumbani mwao badala ulipendekeza kuhifadhiwa benki .

Amesema kuwa utaratibu wa kuhifadhi fedha benki ulikuwa umeandaliwa na kwamba fedha hizo zingegawanywa kwa sehemu husika baada ya miezi mitatu .

Baadhi ya wananchi wa tumbe akiwemo aliyekuwa mwakilishi wa jimbo la tumbe ali bakar bondi amesema halmashauri ni kikwazo katika kuinufaisha jamii ya tumbe na mapato ya soko hilo.

Naye mkuu wa wilaya ya micheweni bi salama mbarouk khatib amewataka wananchi wa tumbe hususani kamati zinazosimamia soko hilo kuangalia uwezekano wa kuzipatia ufumbuzi baadhi ya changamoto ndani ya soko bila ya kutegemea mchango kutoka serikaliani.

No comments