Mkaazi wa Micheweni apandishwa kizimbani kwa tuhuma ya ubakaji
JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba limepandisha katika mahakama ya Wilaya Wete kijana Mwalimu Khamis Suleiman akikabiliwa na tuhuma za kosa la kubaka .
Kijana huyo
mwenye umri wa miaka 22mkaazi wa shehia ya chimba wilaya ya Micheweni ,
anadaiwa kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14.
Imedaiwa
mahakamani hapo na mwendesha mashitaka kutoka Ofisi ya Mkuruguenzi wa mashtaka
wa Serikali ,Juma Ali Juma mbele ya hakimu wa mahakama hiyo abdalla yahya
shamuhuna kwamba mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo siku isiyojulikana ya mwezi
wa tisa mwaka 2017 majira ya saa mbili na nusu usiku huko Chimba alimbaka
mtoto wa kike jina linahifadhiwa .
Baada ya
kusomewa shitaka lake ,mtuhumiwa huyo hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa
mahakama haina uwezo wa kusikiliza kesi za aina hiyo .
Hivyo hakimu wa
mahakama hiyo aliamuru mtuhumiwa huyo amepelekwa rumande hadi kesho asubuhi
atakapopandishwa katika mahakama ya Mkoa .
Post a Comment