Header Ads

Spika wa bunge la China ahutubia mkutano wa mwaka 2018 wa taasisi za Confucius barani Afrika


 
SPIKA wa bunge la China Bw. Li Zhanshu ambaye yupo ziarani nchini Msumbiji na mwenzake wa Msumbiji Veronica Nataniel Macamo wameshiriki kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka 2018 wa taasisi za Confucius barani Afrika uliofanyika jana mjini Maputo. 

Bi. Macamo amesema, mafunzo ya lugha na utamaduni wa kichina yana maana kubwa katika kusukuma mbele maendeleo ya uchumi na jamii ya Msumbiji. Anatarajia mkutano huo utatoa uzoefu zaidi kuzisaidia nchi mbalimbali kueneza mafunzo ya kichina. 

Kwa upande wake, Bw. Li amesema, ushirikiano wa sekta mbalimbali kati ya China na Afrika uko kwenye kiwango cha juu. Anatarajia pande hizo mbili kuendelea na ushirikiano huo mzuri, kujitahidi kwa pamoja kuongeza kiwango na ubora wa mafunzo ya vituo vya Confucius, na kushiriki kwenye ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, ili kutoa mchango kwenye kuhimiza mawasiliano ya elimu ya China na Afrika. 

Pia kuongeza maelewano na urafiki kati ya watu wa pande hizo mbili, kusukuma mbele kujenga kwa jumuiya ya China na Afrika yenye hatma moja na kusadia maendeleo ya utamaduni mbalimbali duniani.

No comments