Mtuhumiwa Dawa za kulevya Kete 688 Kas-Pemba aachiwa huru, Mahakama yataja sababu
MAHAKAMA
Ya Mkoa Wa Kaskazini Pemba imemwachia huru Shibu Ali Juma 35 wa Limbani
Wilaya ya Wete aliyekuwa anakabiliwa na Shitaka la kupatikana na Dawa za
kulevya aina ya Heroin Kete 688 zenye uzito wa Gramu 3.38 .
Hakimu
wa Mahakama hiyo Makame Mshamba Simgeni amesema uwamuzi wa Mahakama kumuachia
huru Mtuhumiwa ni baada ya kubaini kuwa taratibu za ukamataji hazikuzingatiwa.
Aidha
Hamiku Mshamba Ametaja kasoro nyengine ni kuwa Hati ya Upekuzi haikuandikwa
kile kilichokamatwa baada ya Upekuzi uliofanywa na Askari Nyumbani kwa
Mtuhumiwa.
Aidha
Hakimu huyo ameagiza Kuharibiwa vielelezo vyote vya kesi hiyo.
Post a Comment