'Utumiaji wa Dawa za kulevya kwa Vijana umekithiri kila mitaa Pemba'
WANANCHI katika Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, Wametakiwa
Kushirikiana Kwa Pamoja Katika Mitaa yao ili kuweza kutoa taarifa sehemu
husika pale wanapo baini kuwepo kwa viashiria vya matumizi ya Dawa za kulevya.
Hayo yamesemwa na sheha wa Shehia ya Miembeni, Haji Shomari Haji katika mahojiano maalumu na Redio
jamii Micheweni, juu ya suala la kuwepo kwa ongezeko la utumiaji wa Dawa za
kulevya katika shehia hiyo.
Kwa upande wake Afisa Elimu kutoka Tume ya kuratibu na Udhibiti wa Dawa za
Kulevya Kassim Ali Simai, amesema
utumiaji wa Dawa za kulevya kwa Vijana umekithiri kwa kila mitaa na kuwa vijana wengi wameathirika kutokana na matumizi
ya dawa hizo.
Ahmed Abdul Rahman ni Mmoja kati ya Vijana walioathirika na
matumizi ya Dawa hizo amesema makundi ya vijana ndiyo yalimpelekea kujiingiza katika uvutaji wa Dawa hizo na hatimaye kupoteza mwelekeo wa Ndoto zake.
Post a Comment